Pata programu kutoka kwenye Google Play
Unahitaji kuongeza akaunti ya Google kwenye simu yako ili utumie huduma za Google Play. Mabadiliko yanaweza kutumika kwa baadhi ya maudhui yanayopatikana kwenye Google Play. Ili kuongeza mbinu ya malipo, gusa Play Store, gusa nembo yako ya Google kwenye sehemu ya utafutaji, na kisha uguse Mbinu za malipo. Hakikisha kila wakati una kibali kutoka kwa mmiliki wa mbinu ya malipo wakati unanunua maudhui kutoka Google Play.
Ongeza akaunti ya Google kwenye simu yako
- Gusa Mipangilio > Akaunti > Ongeza akaunti > Google. Ukiulizwa, thibitisha mbinu ya kufunga kifaa chako.
- Andika hati tambulishi za akaunti yako ya Google na uguse Ifuatayo, au, kuunda akaunti mpya, gusa Unda akaunti.
- Fuata maagizo kwenye simu yako.
Pakua programu
- Gusa Play Store.
- Gusa upau wa utafutaji ili utafute programu, au chagua programu kutoka kwenye mapendekezo yako.
- Katika ufafanuzi wa programu, gusa sakinisha ili upakue na usakinishe programu.
Ili kuona programu zako, nenda kwenye skrini ya mwanzo na utelezeshe juu kutoka chini ya skrini.