Mwongozo wa mtumiaji wa HMD SKYLINE

Skip to main content
All Devices
Download

HMD SKYLINE

Download

Maelezo ya betri na chaja

Maelezo ya betri na chaja

Ili ukague ikiwa simu yako ina betri inayoweza kuondolewa au isiyoweza kuondolewa, angalia mwongozo uliochapishwa.

Vifaa vilivyo na betri inayoweza kuondolewa Tumia kifaa chako na betri halisi tu inayoweza kuchajiwa upya. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko kawaida, badilisha betri.

Vifaa vilivyo na betri isiyoweza kuondolewa Usijaribu kuitoa betri, kwa sababu unaweza kuharibu kifaa. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko kawaida, kubadilisha betri, peleka kifaa hicho kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa kilicho karibu.

Chaji kifaa chako na chapa inayotangamana. Aina ya plagi ya chaja huenda ikatofautiana. Muda wa kuchaji unaweza kutofautiana kulingana na uwezo wa kifaa.

Maelezo ya usalama wa betri na chaja

Kifaa chako kikikamiliza kuchajiwa, chomoa chaja kutoka kwenye kifaa na soketi ya umeme. Tafadhali kumbuka kwamba kuchaji kwa mfululizo hakupaswi kuzidi saa 12. Ikiachwa bila kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.

Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo na maisha ya betri. Daima jaribu kuweka betri kwenye halijoto kati ya 15°C na 25°C (59°F na 77°F) kwa utendakazi bora. Kifaa chenye betri moto au baridi kinaweza kisifanye kazi kwa muda. Kumbuka kwamba huenda betri ikaisha haraka katika halijoto baridi na kupoteza nishati ya kutosha na kuzima simu katika dakika chache. Ukiwa nje katika halijoto baridi, weka simu yako ikiwa na joto kiasi.

Tii sheria za eneo lako. Peleka ichakatwe upya ikiwezekana. Usitupe kama takataka za kawaida za nyumbani.

Usiweke betri kwenye shinikizo la chini sana la hewa au kuiwacha kwenye halijoto ya juu sana, kwa mfano kuitupa kwenye moto, kwa kuwa hiyo inaweza kusababisha betri kulipuka au kuvuja kiowevu au gesi inayoweza kuwaka moto.

Usifungue, kukata, kuvunja, kukunja, kutoa, au kuharibu betri kwa njia yoyote ile. Kama betri itavuja, usiruhusu umaji uguse ngozi au macho. Hii ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika mara moja na maji, au tafuta msaada wa kitabibu. Usirekebishe, kujaribu kuingiza vitu vigeni kwenye betri, au kuizamisha au kuiweka kwenye maji au aina nyingine ya umaji. Betri zinaweza kulipuka kama zimeharibika.

Tumia betri na chaja kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Matumizi mabaya, au matumizi yasiyoidhinishwa au yasiyotangamana na betri au chaja huenda yakaleta hatari ya moto, mlipuko au hatari nyingine, na huenda ikabatilisha uhalali wowote ulioidhinishwa au waranti. Kama unaamini betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa kituo cha huduma au muuza simu yako kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe usitumie betri au chaja yoyote iliyoharibika. Tumia chaja ndani ya nyumba tu. Usichaji kifaa chako wakati wa dhoruba ya radi. Wakati chaja haijajumuishwa katika furushi la mauzo, chaji kifaa chako kwa kutumia kebo ya data (iliyojumuishwa) na adapta ya nishati ya USB (inaweza kuuzwa kando). Unaweza kuchaji kifaa chako na kebo za wahusika wengine na adapta za nishati ambazo zinatangamana na USB 2.0 au baadaye na kanuni husika za nchi na viwango vya usalama vya kimataifa na mkoa. Huenda adapta nyingine zisitimize viwango husika vya usalama, na kuchaji kwa kutumia adapta hizo kunaweza kusababisha hatari ya kupoteza mali au majeraha ya kibinafsi.

Ili kuchopoa chaja au kifaa chochote cha ziada, kamata na uvute plagi na siyo waya.

Kwa kuongezea, zifuatazo hutumika ikiwa kifaa chako kina betri inayoweza kuondolewa:

  • Zima kifaa kila wakati na chomoa chaja kabla ya kuondoa vifuniko au betri.
  • Mkato wa umeme unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha chuma kitagusa vipapi vya chuma kwenye betri. Huenda hii ikaharibu betri au kifaa kile kingine.
Did you find this helpful?

Useful Links

Software UpdatesFull SpecificationsEnvironmental Profile
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza SIM na kadi za kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
  • Tumia eSIM yako
Maelezo ya bidhaa na usalama
  • Kwa usalama wako
  • Huduma za mtandao na gharama
  • Simu za dharura
  • Kuhudumia kifaa chako
  • Uchakataji upya
  • Alama ya pipa iliyo na mkato
  • Maelezo ya betri na chaja
  • Watoto wadogo
  • Nickel
  • Vifaa vya matibabu
  • Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa
  • Vifaa vya kusaidia kusikia
  • Linda mtoto wako dhidi ya vitu vyenye madhara
  • Magari
  • Mazingira yanayoweza kulipuka
  • Habari ya utoaji cheti
  • Kuhusu Usimamiaji haki za Dijitali
  • Hakimiliki na ilani nyingine

Set Location And Language