Kwa kuwa vifaa vyenye teknolojia pasi waya ya Bluetooth huwasiliana kwa kutumia mawimbi ya redio, havihitaji kuwa vinaangaliana. Hata hivyo, lazima vifaa vyako vya Bluetooth viwe mita 10 (futi 33) na kifaa kile kingine, ijapokuwa muunganisho unaweza kuathiriwa na vizuizi kama vile kuta au kutoka vifaa vingine vya elektroniki.
vifaa vilivyolinganishwa vinaweza bado kuunganishwa kwenye simu yako wakati Bluetooth imewashwa. Vifaa vingine vinaweza kugundua simu yako tu ikiwa mwonekano wa mipangilio ya Bluetooth imefunguliwa.
Usilinganishe au kukubali maombi ya muunganisho kutoka kwa kifaa kisichojulikana. Hii husaidia kulinda simu yako dhidi ya maudhui mabaya.
Ikiwa unataka kushiriki picha zako au maudhui mengine na rafiki, zitume kwenye simu ya rafiki yako kwa kutumia Bluetooth,
Unaweza kutumia zaidi ya muunganisho mmoja wa Bluetooth kwa wakati mmoja. Kwa mfano, wakati unatumia vifaa vya sauti vya Bluetooth, unaweza bado kutuma vitu vingine kwenye simu nyingine.
Msimbosiri hutumika tu wakati unaunganisha kwenye kifaa fulani kwa mara ya kwanza.
Ikiwa huna kifaa ulichooanisha na simu yako, unaweza kuondoa uoanishaji huo.