Upatikani wa baadhi ya bidhaa, vipengele, programu na huduma zilizofafanuliwa katika mwongozo huu zinaweza kutofautiana kulingana na eneo na uhitaji uamilishaji, kujisajili, mtandao na/au muunganisho wa intaneti na mpango unaofaa wa huduma. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mchuuzi au mtoa huduma wako. Kifaa hiki kinaweza kuwa na bidhaa, teknolojia au programu ambayo inaathiriwa na sheria na kanuni za usafirishaji nje ya nchi kutoka Marekani na nchi nyingine. Uchepushaji kinyume na sheria ni marufuku.
Yaliyomo katika waraka huu yametolewa "kama yalivyo". Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila kutoa taarifa kwanza.
Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.
Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global. HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.
HMD Global haitoi wakilishi wowote, waranti au kuwajibika kwa utendaji kazi, maudhui, au usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika wa tatu zilizotolewa na kifaa chako. Kwa kutumia programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.
Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji taswira na video huenda ukajumuisha upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa upitishaji data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana kimaeneo. Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa chaguo za lugha.
Vipengele, utendakazi na ainisho nyingine za bidhaa zinaweza kutegemea mtandao na hutegemea masharti, sheria, na gharama za ziada.
Ainisho, vipengele na maelezo mengine yote ya bidhaa yaliyotolewa yanaweza kubadilishwa bila ilani.
Sera ya Faragha ya HMD Global, inayopatikana kwenye https://www.hmd.com/privacy, inatumika kwa matumizi yako ya kifaa.
TM na © 2024 HMD Global. Haki zote zimehifadhiwa.
Android, Google na alama na nembo zingine husika ni alama za biashara za Google LLC.
Alama ya neno na nembo za Bluetooth zinamilikiwa na Bluetooth SIG, Inc. na matumizi yoyote ya alama hizo na HMD Global yako chini ya leseni.
OZO ni alama ya biashara Nokia Technologies Oy.
Alama ya Qi2 ni alama ya biashara ya Wireless Power Consortium.
Bidhaa hii ina sumaku na inatii Kiwango kipya cha Wasifu wa Sumaku wa Qi v2.0.
Tumia chaja zinazotangamana na Qi2 pekee ili kuchaji pasiwaya.
Qi ID 21201 (TA-1600) na 21649 (TA-1688).