Mwongozo wa mtumiaji wa HMD SKYLINE

Skip to main content
All Devices
Download

HMD SKYLINE

Download

Tumia skrini ya mguso

Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu kingine chenye ncha kali kwenye skrini ya mguso.

Gusa na ushikilie ili kukokota kipengee

Gusa na ushikilie ili kukokota kipengee

Weka kidole chako kwenye kipengee kwa sekunde chache, na utelezeshe kidole chako kwenye skrini.

Pitisha

Pitisha

Weka kidole chako kwenye skrini, na utelezeshe kidole chako kwenye mweleko unaotaka.

Tembeza kwenye orodha au menyu ndefu

Tembeza kwenye orodha au menyu ndefu

Telezesha kidole chako kwa haraka katika mwelekeo wa juu au chini kwenye skrini, na uinue kidole chako. Ili kukomesha kutembeza, gusa skrini.

Kuza ndani au nje

Kuza ndani au nje

Weka vidole 2 kwenye kipengee, kama vile ramani, picha, au ukurasa wavuti, na utelezeshe vidole vako vikiwa kando au pamoja.

Funga mwelekeo wa skrini

Telezesha chini kuanzia juu ya skrini, na uguse Zungusha kiotomatiki > Washa. Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.

Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse Zungusha kiotomatiki > Zima.

Rambaza kwa kutumia ishara

Kuwasha kwa kutumia urambazaji wa ishara, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Hali ya urambazaji > Urambazaji wa ishara.

  • Ili kuona programu zako zote, kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kwenye skrini.
  • Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kutoka chini ya skrini. Programu uliyokuwa ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
  • Kuona programu gani umefungua, telezesha juu kutoka chini ya skrini bila kutoa kidole chako hadi uone programu, kisha uondoe kidole chako. Ili kubadilisha kwa programu nyingine iliyofunguliwa, gusa programu. Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa, telezesha kulia kupitia programu zote na uguse FUTA ZOTE.
  • Ili urudi kwenye skrini ya awali ambayo ulikuwa unatumia, telezesha kutoka upande wa kulia au kushoto ya skrini. simu yako hukumbuka programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.

Rambaza kwa kutumia vitufe

Kuwasha vitufe vya urambazaji, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Hali ya urambazaji > Urambazaji wa vitufe 3.

  • Ili kuona programu zako zote, kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kuanzia chini ya skrini.
  • Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa circle. Programu uliyokuwa ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
  • Ili kuona ni programu gani ulizofungua, gusa stop. Ili kubadilisha kwa programu nyingine iliyofunguliwa, telezesha kulia na uguse programu. Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa, telezesha kulia kupitia programu zote na uguse FUTA ZOTE.
  • Ili kurudi kwenye skrini iliyotangulia uliyokuwa, gusa . simu yako hukumbuka programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
Did you find this helpful?

Useful Links

Software UpdatesFull SpecificationsEnvironmental Profile
Anza kutumia
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza SIM na kadi za kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
  • Tumia eSIM yako

Set Location And Language