Shughulikia kifaa chako, betri, chaja na vifaa vya ziada kwa uangalifu. Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia kufanya kifaa chako kifanye kazi.
- Weka kifaa kikiwa kikavu. Taka za mtuamo, unyevu wa hewa, na aina zote za vimiminiko au unyevu zinaweza kuwa na madini yanayoweza kutia kutu saketi za elektroniki.
- Usitumie au kuhifadhi kifaa chako kwenye maeneo yenye vumbi au uchafu.
- Usihifadhi kifaa kwenye halijoto ya juu au ya chini. Halijoto ya juu huenda ikaharibu kifaa au betri.
- Usihifadhi kifaa kwenye halijoto baridi. Wakati kifaa kimerudi kwenye joto lake la kawaida, unyevunyevu unaweza kutengenezeka ndani ya kifaa.
- Usifungue kifaa kando na ilivyoagizwa katika kiongozi cha mtumiaji.
- Marekebisho ambayo hayajaidhinishwa yanaweza kuharibu kifaa na kukiuka kanuni zinazosimamia vifaa vya redio.
- Usiangushe, kugonga au kutingisa kifaa au betri. Kukishika kiholela kunaweza kuivunja.
- Tumia kitambaa laini, kisafi na kikavu kusafisha uso wa kifaa hiki.
- Usipake rangi kifaa. Rangi inaweza kuzuia utendaji kazi wa kawaida.
- Weka kifaa chako mbali na sumaku au maeneo ya sumaku.
- Ili kuweka data yako muhimu salama, ihifadhi angalau katika maeneo mawili tofauti, kama vile kifaa chako, kadi ya kumbukumbu, au kompyuta au andika maelezo muhimu.
Wakati wa utendajikazi kwa muda mrefu, kifaa kinaweza kuwa na joto. Katika hali nyingi, hii ni kawaida. Kuepuka kupata joto sana, huenda kifaa kikapunguka kasi kiotomati, kikapunguza mwangaza wakati wa simu ya video, kikafunga programu, kikazima kuchaji, na ikiwezekana, kikajizima chenyewe. Kama kifaa hakifanyi kazi vizuri, kipeleke kwenye suhula iliyo karibu ya huduma iliyoidhinishwa.