Mwongozo wa mtumiaji wa HMD Skyline

Skip to main content
We need a better phone for our mental health. Learn more about The Better Phone Project and join our discussion "Attention and finding balance"
All Devices
Download

HMD Skyline

Download

Chaji simu yako

Chaji betri

Chaji betri
  1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
  2. Unganisha kebo kwenye simu yako.

Unaweza kuchaji simu yako kwa kutumia chaja pasiwaya. Tumia chaja zinazotangamana na Qi pekee ili kuchaji pasiwaya.

Simu yako inakubali kebo ya USB ya C. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.

Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji kuonyeshwa.

Modeli ya chaja

Chaji kifaa chako kwa chaja ya HHAD-033N. HMD Global inaweza kutengeneza modeli za ziada za betri au chaja zipatikane kwa kifaa hiki. Muda wa kuchaji unaweza kutofautiana kulingana na uwezo wa kifaa. Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa cha kichwani, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.

Wakati chaja haijajumuishwa katika furushi la mauzo, chaji kifaa chako kwa kutumia kebo ya data (iliyojumuishwa) na adapta ya nishati ya USB (inaweza kuuzwa kando). Unaweza kuchaji kifaa chako na kebo za wahusika wengine na adapta za nishati ambazo zinatangamana na USB 2.0 au baadaye na kanuni husika za nchi na viwango vya usalama vya kimataifa na mkoa. Huenda adapta nyingine zisitimize viwango husika vya usalama, na kuchaji kwa kutumia adapta hizo kunaweza kusababisha hatari ya kupoteza mali au majeraha ya kibinafsi. Inapendekezwa utumie adapta ya nishati yenye ingizo la 100-240V~50/60Hz 0.8A na towe ya 15.0V/2.2A ili kuboresha kuchaji kifaa chako.

Did you find this helpful?

Useful Links

Software UpdatesFull SpecificationsEnvironmental Profile
Anza kutumia
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza SIM na kadi za kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
  • Tumia eSIM yako

Set Location And Language