Soma maelekezo haya rahisi. Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au kinyume cha sheria na masharti. Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo kamili wa mtumiaji.
Zima kifaa wakati matumizi ya kifaa cha mkononi yamekatazwa au wakati yanaweza kusababisha mwingiliano au hatari, kwa mfano, ndani ya ndege au hospitalini, au karibu na vifaa vya matibabu, mafuta, kemikali, au maeneo yenye mlipuko. Tii maagizo yote katika maeneo yaliyozuiwa.
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima iache mikono yako iwe huru kuendesha gari. Kitu cha kuzingatia kwanza unapoendesha gari unapaswa kuwa usalama barabarani.
Vifaa vyote visivyotumia waya vina uwezekano wa kupata mwingiliano, ambao unaweza kuathiri utendaji kazi wake.
Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kuweka au kukarabati bidhaa hii.
Tumia betri, chaja, na vifaa vya ziada ambavyo vimeidhinishwa na HMD Global Oy kwa ajili ya matumizi na kifaa hiki tu. Usiunganishe bidhaa ambazo hazitangamani.
Ikiwa kifaa chako kinazuia maji, angalia ukadiriaji wake wa IP katika ainisho za kiufundi za kifaa kwa maelekezo zaidi tondoti.
Kifaa na/au skrini yake imetengenezwa kwa glasi. Glasi hii inaweza kuvunjika kifaa kikiangushwa mahali pagumu au kupokea mgongano mzito. Glasi ikivunjika, usiguse sehemu za glasi za kifaa au ujaribu kuondoa glasi iliyovunjika kutoka kwa kifaa. Acha kutumia kifaa hadi glasi ibadilishwe na mhudumu aliyeidhinishwa.
Kuzuia madhara yanayowezekana ya kusikia, usisikilize katika viwango vya juu vya sauti kwa muda mrefu. Kuwa mwangalifu wakati unashikilia kifaa chako karibu na sikio wakati kipaza sauti kinatumika.