Zima kifaa chako katika eneo lolote lenya mazingira yanayoweza kulipika, kama vile karibu na pampu za mafuta katika vituo vya mafuta. Cheche zinaweza kusababisha mlipuko au moto unaoweza kuleta majeraha au kifo. Kumbuka vikwazo katika maeneo yenye mafuta; viwanda vya kemikali; au mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye mazingira yenye uwezekano wa milipuko yanaweza kuwa na alama zisizo dhahiri. Haya kwa kawaida ni maeneo ambapo unaweza kushauriwa kuzima injini yako, chini ya sitaha kwenye boti, uhamishaji kemikali au suhula za kuhifadhi, na ambapo hewa ina kemikali au chembechembe kama vile nafaka, vumbi au poda ya chuma. Wasiliana na watengenezaji wa magari yanayotumia mafuta aina ya gesi oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile propeni au buteni) ikiwa kifaa hiki kinaweza kutumiwa vizuri katika maeneo yao.