Kifaa chako kinaweza kupata virusi na vitu vingine vyenye madhara. Chukua tahadhari zifuatazo:
Kuwa mwangalifu unapofungua ujumbe. Huenda zikawa na programu mbaya au yenye kudhuru kifaa au kompyuta yako.
Kuwa mwangalifu unapokubali maombi ya muunganisho, kuvinjari mtandao, au kupakua maudhui. Usikubali miunganisho ya Bluetooth kutoka kwenye vyanzo usivyoviamini.
Sakinisha tu na utumie huduma na programu kutoka kwa vyanzo unavyoamini na vinavyotoa usalama na ulinzi wa kutosha.
Sakinisha antivirus na programu nyingine za usalama kwenye kifaa chako na kompyuta yoyote iliyounganishwa. Tumia tu programu moja ya kinga virusi kwa wakati mmoja. Kutumia zaidi ya moja huenda kukaathiri utendakazi na utumizi wa kifaa na/au kompyuta.
Ikiwa unafikia vialamisho vilivyosakinishwa mapema na viungo kwa tovuti vya mhusika wa tatu, chukua tahadhari zinazohitajika. HMD Global haiidhinishi wala kuwajibika kwa tovuti hizo.