Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana huenda yakaharibu kadi au kifaa, na huenda yakaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
SIM kadi zote zinapatikana kwa wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini ijapokuwa SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, kwa kupiga simu, ile nyingine haipatikani.
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Ikiwa una eSIM kadi badala ya SIM kadi halisi, washa simu yako na ufuate maagizo kwenye simu. Kuweza kuamilisha eSIM yako, unahitaji muunganisho wa Wi-Fi. Ili kununua eSIM kadi, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao. Kumbuka kwamba ikiwa una simu ya SIM-moja, unaweza kuwa na SIM kadi moja tu, ya halisi au eSIM, inayotumika kwa wakati mmmoja. Kumbuka kwamba ikiwa una simu ya SIM-mbili, unaweza kuwa na SIM kadi mbili halisi au SIM halisi na eSIM inayotumika kwa wakati mmmoja. Kwa maelezo zaidi kuhusu eSIM kadi, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.